

Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) imeshiriki kwa mafanikio katika Maonesho ya Pili ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar 2025, yanayofanyika katika viwanja vya Dimani, Fumba Zanzibar, na kufunguliwa rasmi na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga.
Kupitia ushiriki wake, NCAA imeendelea kuimarisha uelewa wa umma kuhusu umuhimu wa uhifadhi, utalii na fursa za uwekezaji zinazopatikana Hifadhi ya Ngorongoro ambalo ni eneo la kipekee duniani linalotambuliwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia.
Akizungumza katika banda la NCAA, Bi. Zuhura Khalifa, mkazi wa Mkwajuni, aliipongeza mamlaka hiyo kwa kuleta elimu ya uhifadhi na taarifa za huduma za utalii katika visiwa vya Zanzibar.
“Watu wengi wamekuwa wakisikia kuhusu Hifadhi ya Ngorongoro, lakini hawakuwa na taarifa sahihi kuhusu huduma zake. Ushiriki wa NCAA katika maonesho haya umetufungua macho na umetufundisha mengi,” alieleza kwa furaha.
Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa NCAA, Mustapha Seifdine, alitoa shukrani kwa wananchi wote waliotembelea banda la mamlaka hiyo, akisisitiza kuwa ushiriki wa NCAA katika maonesho hayo ni muendelezo wa kusambaza taarifa sahihi kuhusu vivutio vya utalii na juhudi za uhifadhi.
“Tumejipanga kwa mkakati wa muda mrefu, si tu kutangaza vivutio vya Ngorongoro, bali pia kutoa elimu ya uhifadhi kwa wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo nchini kote. Lengo letu ni kuhakikisha kaulimbiu ya ‘Tumerithishwa, Tuwarithishe’ inakuwa ya vitendo na endelevu,” alieleza Mustapha.
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI