

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile (Mb), amesema kuwa uwazi na uwajibikaji ni nguzo muhimu katika kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinatumika kwa tija na kwa faida ya wananchi wote, huku akiwataka watumishi wa umma kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda maslahi ya taifa.
Kauli hiyo imepokelewa kwa uzito na viongozi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU waliokuwa wakishiriki maonesho hayo, wakiahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na wizara zote katika kusimamia matumizi ya fedha na kuhakikisha miradi yote inaendeshwa kwa uwazi na kufuata taratibu.
Akizungumza leo Juni 19, 2025, katika banda la TAKUKURU kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma, Mhe. Kihenzile ameeleza kuwa mwaka huu una umuhimu mkubwa kisiasa na kijamii, hivyo ni jukumu la taasisi kama TAKUKURU kuhakikisha nidhamu ya fedha inazingatiwa kikamilifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Aidha amesema kuwa Serikali haitavumilia miradi yoyote inayoisimamia iwapo itabainika kuwa na viashiria vya rushwa, akisisitiza kuwa rushwa ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya Taifa.
“Miradi yote tunayoisimamia kama ina harufu ya rushwa haitakamilika. Na mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, tunawatakia heri TAKUKURU mtusimamie vizuri ili tupate viongozi bora na waadilifu,” alisema Mhe. Kihenzile mbele ya viongozi wa taasisi hiyo na wadau wengine wa sekta ya usafirishaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Uelimishaji Umma TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Faustine Malecha amesema wamethibitisha kuwa wataendelea kutumia jukwaa la Wiki ya Utumishi wa Umma kutoa elimu kuhusu rushwa katika maeneo mbalimbali, na kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi kwa uadilifu na bila kushawishiwa kwa rushwa.
“TAKUKURU tumekuja hapa kutoa elimu kuhusu madhara ya kutoa na kupokea rushwa tunawaelimisha wananchi ili kuhakikisha kwamba hawachagui viongozi wanaonunua nafasi kwa kutoa rushwa kwa sababu viongozi wa aina hiyo hawawezi kuwaletea maendeleo,” amesema
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI