KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI

Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2025, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile (Mb), ametembelea banda la Wizara ya Uchukuzi katika Viwanja vya Chinangali Dodoma, ambapo amepongeza jitihada za watumishi wa sekta hiyo kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
19 Jun 2025
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI

Akizungumza na watendaji wa wizara hiyo, leo June 19,2025  Kihenzile amesema Wiki ya Utumishi wa Umma ni fursa muhimu ya kujifunza, kusikiliza wananchi, na kuboresha mifumo ya utoaji huduma, hasa katika sekta ya uchukuzi ambayo ndiyo mhimili wa maendeleo ya kiuchumi.

“Sekta ya uchukuzi inagusa maisha ya kila Mtanzania  iwe ni kwenye reli, barabara, anga au usafiri wa majini tunahitaji kuendelea kujenga mfumo unaomuweka mwananchi mbele kwa kuhakikisha huduma ni za haraka, salama, na zenye tija,” amesema.

Ameongeza kuwa maonesho hayo yanaongeza uwazi na uelewa kwa wananchi kuhusu huduma zinazotolewa na Wizara ya Uchukuzi, sambamba na kuwaweka karibu zaidi na Serikali yao.

“Katika wiki hii, tunapaswa kujiuliza kama tunamtumikia mwananchi kwa uadilifu na ufanisi,Watumishi wa umma tuna jukumu la kuakisi maadili ya uwajibikaji, uvumilivu na ubunifu kwa manufaa ya Taifa letu,” amesisitiza Kihenzile.

Ziara ya Naibu Waziri imeleta hamasa kwa wadau waliotembelea banda hilo, huku watendaji wa wizara wakiahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa kuzingatia dira ya maendeleo ya uchumi wa viwanda na usafirishaji endelevu.

Watu 36 Wafariki Dunia, Majeruhi 23 Wakimbizwa Hospitali

Watu 36 Wafariki Dunia, Majeruhi 23 Wakimbizwa Hospitali

Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.

Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.

Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma

Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma

Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake

Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake