

Mchungaji Richard Hananja ameonya vikali tabia ya baadhi ya viongozi wa dini kutumia majukwaa ya kidini kwa ajili ya kujitafutia umaarufu kupitia matukio ya utekaji au kupotea kwa watu nchini.
Mchungaji Richard Hananja ameonya vikali tabia ya baadhi ya viongozi wa dini kutumia majukwaa ya kidini kwa ajili ya kujitafutia umaarufu kupitia matukio ya utekaji au kupotea kwa watu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mchungaji Hananja amesema hakuna dini wala mtu mwenye maadili anayeweza kufurahishwa na matukio ya watu kutekwa au kupotea. Amesisitiza kuwa suluhu ya kweli ya changamoto hizo haiwezi kupatikana kwa maneno ya jukwaani bali kupitia vikao halali vya mazungumzo.
Aidha, amewataka viongozi wa dini kuacha kuishutumu serikali na vyombo vya ulinzi kwa tuhuma zisizo na msingi huku akisisitiza kuwa vyombo hivyo vinafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.
Aidha ametoa wito kwa Watanzania kuwa na subira na hekima, na kuepuka kujihusisha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani ya nchi.
Mchungaji Hananja pia amehoji sababu ya chokochoko kuibuka kila taifa linapokaribia uchaguzi mkuu, akidai kuwa mara nyingi hali hiyo hutumiwa na baadhi ya watu kwa manufaa ya kisiasa. Ametahadharisha kuwa mwenendo huo unaweza kuhatarisha mshikamano wa kitaifa.
Katika hatua nyingine, Mchungaji Hananja amesisitiza umuhimu wa mazungumzo kati ya pande zinazohusika, akieleza kuwa hata maandiko ya kidini yanahimiza matumizi ya “kiti na meza” kama njia ya kuleta suluhu ya kweli katika jamii
Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum
DIB YAHIMIZA WANANCHI KUDAI FIDIA ZAO KUTOKA BENKI ZILIZOFILISIKA
USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA
DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA
BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.
Aliyeongoza kura maoni Vunjo 2020, kumkabili tena Dkt. Kimei
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma