Ilani Ya CCM Imeandaliwa Kwa Weledi Mkubwa Kwa Kushirikiana Na Wananchi;RAIS Dkt.Samia | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

Ilani Ya CCM Imeandaliwa Kwa Weledi Mkubwa Kwa Kushirikiana Na Wananchi;RAIS Dkt.Samia

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesemaamewahakikishia wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum Taifa kwamba Ilani ya Chama hicho imeandaliwa kwa weledi mkubwa na imeandaliwa kwa kuwashirikisha wananchi wenyewe, asasi za kiraia, taasisi za elimu ya juu na wadau wengine wengi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
29 May 2025
Ilani Ya CCM Imeandaliwa Kwa Weledi Mkubwa Kwa Kushirikiana Na Wananchi;RAIS Dkt.Samia

Ameeleza kuwa Ilani ya Chama hicho imeandaliwa kwa weledi mkubwa na imeandaliwa kwa kuwashirikisha wananchi wenyewe, asasi za kiraia, taasisi za elimu ya juu na wadau wengine wengi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii.

Mwenyekiti huyo amesema hayo leo jijini hapa wakati akizindua mkutano huo ambapo amesema kesho watafanya  uzinduzi wa Ilani ya Chama hicho ya uchaguzi ya mwaka 2025/2030 ambayo itakayokwenda kuinadi kwa wananchi ili wawape imani na ridhaa ya kuwarudisha kuendeIea kuwa  serikalini katika kipindi kingine cha miaka mitano.


Dkt. Samia amesema Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 iliakisi kipindi cha kwanza cha miaka mitano utekelezaji wa mwelekeo wa sera za Chama hicho katika kipindi cha miaka 2020/2030.

Amesema Ilani ya uchaguzi ya mwaka huu inaakisi kipindi cha pili cha utekelezaji wa mwelekeo wa sera za CCM katika kipindi cha mwaka 2020 hadi mwaka 2030 huko akisema kabla wanaendelea mbele wameona ni muhimu kufanya tena mapitio ya utekelezaji wa Ilani iliyopita ya miaka mitano. Na ndio kazi tutakayoifanya leo na kesho tunawasilisha Ilani hiyo wanayokwenda nayo inavitu gani ndani na tutaizindua rasmi.

Ameeleza kuwa matarajio yake baada ya kupokea taarifa za serikali za utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho ya uchaguzi Mkuu ya mwaka 2020/2025 pamoja na uzinduzi rasmi wa Ilani ya uchaguzi Mkuu hiyo mpya wajumbe wote wa mkutano Mkuu Maalum kwa pamoja watabeba jukumu la kufikisha na kuitangaza kwa wananchi wakati utakapofika.

Amesema jukumu hilo litakuwa sambamba na kuyatangaza kwa wananchi mafanikio yaliyofikiwa na CCM katika utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025.

Amesema katika kuendelea na jitihada za kujenga Chama hicho ambapo alitumia fursa kuwajukisha wajumbe hao kuwa Mei 28,mwaka huu alipata fursa ya kuweka jiwe la msingi la makao makuu ya CCM na ofisi zake.

"Ninafurahi kuwaona wajumbe wote mkiwa wenye nyuso za bashasha ninashukuru sana kwa mahudhurio yenu mazuri nyinyi pamoja na wageni wetu waalikwa nimepata mapokezi mazuri, nawashukuru sana wageni wetu waalikwa kuja kuungana na sisi," amesema.

Amesema uwepo wao ni udhibitisho tosha ni mapenzi ya dhati ya kudumisha undugu, urafiki, Umoja  na mshikamano baina ya vyama vyao na wananchi wa mataifa yao.

"Ndugu wajumbe wa mkutano Mkuu mtakumbuka kwamba mkutano maalum wa Januari 18 na 19, 2025 tulipokea taarifa ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa kuhusu utekelezaji wa kazi za Chama na Jumuiya zake kwa kipindi cha mwaka 2020 /2024," alisema Mwenyekiti huyo.

Amesema walipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 kwa kipindi cha miaka minne yaliyofanywa na serikali zote mbili Tanzania Bara na Zanzibar.

Ameongeza kuwa walifanya marekebisho madogo ya Katiba ya Chama hicho ya mwaka 1977 na likawa toleo la 2020/2025 na kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.

Rais Dkt. Samia amefafanua kuwa mkutano ule kwa kuzingatia ibara ya 100 kifungu kidogo cha pili nanibara ya 101 kifungu cha tano, kifungu kidogo cha b za katiba ya CCM ya mwaka 1977.

" Itakumbukwa kuwa katika kutekeleza jukumu lake la kikatiba lililoainishwa chini ya ibara 103 kifungu kidogo cha 4 ya Katiba ya Chama cha Mapinduzi, Halmashauri kuu ya CCM Taifa katika kikao chake kilichofanyika Dodoma Machi 10, mwaka huu pamoja na mambo mengine ilipokea na kuthibitisha Ilani ya Chama hicho ya uchaguzi ya mwaka huu," alieleza.

Ameeleza kuwa walimaliza kazi ya kumteua mgombea wa nafasi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na mgombea mwenza.

Amesema kuwa walimthibitisha mgombea wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama Chama Mapinduzi.

Ameeleza kuwa mkutano Mkuu huo ni sehemu ya maandalizi ya chama hicho kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2025.

KAPINGA ATAJA VIGEZO VYA ZIADA UPELEKAJI UMEME VITONGOJINI.

KAPINGA ATAJA VIGEZO VYA ZIADA UPELEKAJI UMEME VITONGOJINI.

MINARA 304 YA 2G IMEBORESHWA HADI KUFIKIA 3G/4G-UCSAF.

MINARA 304 YA 2G IMEBORESHWA HADI KUFIKIA 3G/4G-UCSAF.

SERIKALI IMETOA RUZUKU YA ASILIMIA 20 HADI 50 KWENYE MITUNGI YA GESI  LAKI 4.4 – KAPINGA.

SERIKALI IMETOA RUZUKU YA ASILIMIA 20 HADI 50 KWENYE MITUNGI YA GESI LAKI 4.4 – KAPINGA.

SERIKALI YAWATAKA WADAU KUWEKA MAZINGIRA YANAYORUHUSU UBUNIFU.

SERIKALI YAWATAKA WADAU KUWEKA MAZINGIRA YANAYORUHUSU UBUNIFU.

KAPINGA AZINDUA KITUO MAMA CHA GESI ASILIA ILIYOSHINDILIWA (CNG) JIJINI DAR ES SALAAM.

KAPINGA AZINDUA KITUO MAMA CHA GESI ASILIA ILIYOSHINDILIWA (CNG) JIJINI DAR ES SALAAM.