Moto watekeza mitaa, makazi Los Angeles, Marekani | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kimataifa

Moto watekeza mitaa, makazi Los Angeles, Marekani

Los Angeles. Moto mkubwa unaendelea kuteketeza maeneo mbalimbali katika mji Los Angeles, Marekani, huku upepo mkali ukichochea maafa hayo.

Elidaima Mangela
By Elidaima Mangela
08 Jan 2025
Moto watekeza mitaa, makazi Los Angeles, Marekani

Hali hiyo imesababisha mamlaka kuamuru watu zaidi ya 30,000 kuhamishwa kutoka katika maeneo yaliyo hatarini, kwani moto huo unaleta tishio kubwa la kuenea kwa kasi. 
Mkuu wa Zima Moto wa Los Angeles, Kristin Crowley ameeleza kuwa bahati yao ni kwamba mpaka sasa hakuna majeruhi walioripotiwa, huku akiongeza kuwa watu zaidi ya 25,000 katika nyumba 10,000 walikuwa katika hatari.

Hata hivyo, upepo mkali umeonekana kuchangia kuenea kwa moto huo, huku juhudi za zimamoto zikitatizwa na upepo huo.

Wataalamu wanadhihirisha kuwa hali hii ni sehemu ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayoathiri maeneo mengi duniani.

Inaripotiwa kuwa takribani ekari 2,921 za eneo la Pacific Palisades kati ya makazi ya pwani ya Santa Monica na Malibu zilikuwa zimeungua, kama ilivyoelezwa na maofisa wa polisi baada ya kutoa onyo la hatari kubwa ya moto uliosababishwa na upepo mkali uliofuata baada ya hali ya hewa kavu kwa muda mrefu.

Moto ulienea huku maofisa wakionya kwamba hali mbaya ya upepo ilitarajiwa kuja usiku, na kusababisha wasiwasi kwamba mitaa mingi zaidi inaweza kulazimika kuhamishwa.
Hata hivyo, Jiji la Santa Monica baadaye lililazimika kuwahamisha watu katika kingo za Kaskazini za jiji.

Mashuhuda wameliripoti kuwa nyumba kadhaa zilikuwa zikiteketea kwa moto, na majivu yakikaribia kuchoma magari yao wakati watu wakikimbia katika milimani ya Topanga Canyon, huku moto ukienea kutoka huko hadi bahari ya Pasifiki.

Matoaji wa huduma ya dharura katika ndege amesema wamekusanya maji kutoka baharini ili kuyamwaga kwenye moto ulio karibu.

Reuters imeripoti kuwa Moto uliteketeza nyumba na buldoza ziliondoa magari yaliyotelekezwa barabarani ili magari ya dharura yaweze kupita, kama ilivyoonyeshwa kwenye picha za televisheni.

Kadiri jua lilivyoshuka juu ya Los Angeles, miali ya moto ya rangi ya rangi ya machungwa ilitawala vilima vinavyoelekea Topanga.

Moto huo pia ulisababisha uharibifu wa miti kwenye maeneo ya Getty Villa, jumba la makumbusho lenye kazi za sanaa za thamani kubwa, lakini mkusanyiko wa kazi hizo ulisalia salama hasa kutokana na juhudi za kinga za kukata majani yanayozunguka majengo, alisema jumba la makumbusho.

"Wasichana waliacha magari yao Palisades Drive. Moto unateketeza mlima, miti ya mitende - kila kitu kinateketea," amesema Festa kutoka kwenye gari lake.

Kabla ya moto kuanza, Huduma ya Hali ya Hewa ya Kitaifa ilikuwa imetoa tahadhari ya juu zaidi kwa hali ya moto kali kwa sehemu kubwa ya Kaunti ya Los Angeles kuanzia Jumanne hadi Alhamisi, ikitabiri upepo wa kasi ya maili 50 hadi 80 kwa saa.

MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.

MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.

KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI

KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI

MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA

MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA

Maria Sarungi atekwa Kenya wasiojulikana watajwa

Maria Sarungi atekwa Kenya wasiojulikana watajwa