

Bodi ya Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) wameishauri Mamlaka ya Bandari Tanzania kuangalia uwezekano wa kujenga maghala ya kuhifadhia mafuta Bandari ya Mbamba Bay kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji wa mafuta nchi jirani za Malawi na Msumbiji.
Bodi ya Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) wameishauri Mamlaka ya Bandari Tanzania kuangalia uwezekano wa kujenga maghala ya kuhifadhia mafuta Bandari ya Mbamba Bay kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji wa mafuta nchi jirani za Malawi na Msumbiji.
Akizungumza baada ya kutembelea eneo la mradi huo wenye thamani ya bilioni 75.8, Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Lutengano Mwakahesya kwa niaba ya Wajumbe wa Bodi amesema ujenzi wa matanki hayo utasaidia uhifadhi na usafirishaji wa mafuta kwenda nchi jirani za Msumbiji na Malawi yakitokea bandari ya Mtwara kupitia Ziwa Nyasa.
Amesema kuwa ni muhimu TPA ikaweka kipaumbele katika ujenzi wa matenki ya kupokelea na kusafirisha mafuta kwa ajili ya kuongeza pato la nchi pamoja na kusaidia makampuni ya mafuta kupata sehemu ya kuhifadhia mafuta kwa jili ya kusafirisha nchi jirani.
“Tayari PBPA iliwasilisha mapendekezo hayo ya ujenzi wa matenki hayo na tulitarajia kuona ujenzi umeshaanza”amesema Dkt. Mwakahesya
Meneja wa Mipango ya Mafuta Gilbert Jungulu amesema matenki hayo yakiwekwa makampuni ya mafuta yatakuja kwaajili ya kuhifadhi mafuta ya kwenda nchi jirani na kuingizia kipato mamlaka na kazi ya TPA itakuwa ni kuhifadhi ambapo itawaingizia kipato kikubwa.
Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya ameipongeza Bodi ya PBPA kwa kuona fursa ya ujenzi wa matenki katika bandari hiyo kwani utasaidia kuongeza pato la Taifa na kuongezeka kipato kwa wananchi wa jimbo la Nyasa na kuahidi kutoa ushirikiano kuhakikisha ujenzi huo unafanikiwa.
Naye Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Manga Gasaya amewashukuru wajumbe wa bodi kwa kuona umuhimu wa kuongeza mradi wa ujenzi wa matenki na kusema kuwa atawasilisha maoni hayo kwenye mamlaka husika na kusisitiza kuwa bado muda upo wa kuongeza ujenzi huo kwenye mradi wa bandari.
Awali, Mhandisi Mkazi wa mradi huo Agathon Mwenda amesema ttekelezaji wa ujenzi wa bandari hiyo utahusisha ujenzi wa gati mbili,ujenzi wa maghala, nyumba za watumishi, jengo la utawala, jengo la abiria, karakana, mnara wa tanki la maji na jengo la huduma za afya.
Amesema ujenzi pia utahusisha barabara za ndani na nje ya bandari kwa ajili ya magari kuingia na kutoka bandarini hapo na ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 105 na upana wa mita 15 kwa ajili ya magari ya kubebea mizigo na eneo la kuhifadhia makontena 3,000 ya mizigo.
Ujenzi wa bandari mpya ya kisasa ya Mbamba Bay inayojengwa pembezoni mwa Ziwa Nyasa katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma inatarajiwa kukamilika Januari 2026 .Ujenzi wa bandari hiyo mpya unasimamiwa na Mkandarasi Xiamen Ongoing Construction Group Limited na mshauri (Consultant) Anova Consult
WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WAASWA KUZINGATIA MADILI
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI
WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.
SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.
AZANIA BENKI BUNGE BONANZA LAWALETA PAMOJA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA.
MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUKUTANA KATIKA BONANZA LA KUHAMASISHA MICHEZO NA UMUHIMU WA MAZOEZI.
MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.
RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.
WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI