BoT KUJA NA MFUMO WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA KIFEDHA KIDIGITAL. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

BoT KUJA NA MFUMO WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA KIFEDHA KIDIGITAL.

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kuzindua rasmi mfumo wa kidigitali wa utatuzi wa Malalamiko ya kifedha kwa wananchi(FCRS),huku ikitoa rai kwa watoa huduma za kifedha kuhakikisha wanauelewa mfumo huo kwani wao ndio wanaokutana na wananchi moja kwa moja.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
10 Dec 2024
BoT KUJA NA MFUMO WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA KIFEDHA KIDIGITAL.

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kuzindua rasmi mfumo wa kidigitali wa utatuzi wa  Malalamiko ya kifedha kwa  wananchi(FCRS),huku ikitoa rai kwa watoa huduma za kifedha kuhakikisha wanauelewa mfumo huo kwani wao ndio wanaokutana na wananchi moja kwa moja.

Hayo yamesemwa leo Disemba 10,2024Jijini Dar es Salaam, na Kaimu Mkurugenzi wa  Huduma Jumuishi  za Fedha  wa BoT, Nangi Massawe  wakati alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili kuhusu mfumo wa malalamiko kwa wawakilishi wa taasisi za fedha nchini

Amesema mfumo huo utakaomwezesha mtumiaji wa huduma za kifedha kuwasilisha malalamiko kutumia mtandao, unatarajiwa kuanzia Januari mwaka 2025 na mpaka sasa tayari umekamilika kinachofanyika sasa ni kutoa elimu  kwa taasisi za fedha ili kuuelewa vizuri mfumo huo.

Amesema jukumu kubwa la benki kuu ni kuhakikisha inamlinda  mtumiaji wa huduma za kifedha  kuwa na uelewa wa  masuala ya kifedha, kujua ni wapi atawasilisha malalamiko yake na kupata haki, kwani wamekuwa wakifanya hivyo kujenga imani na huduma za kifedha na  kutumia huduma rasmi ili kukamilisha lengo la kuwepo kwa huduma jumuishi.

"Mfumo umetengenezwa na kukamilika, tunaamini ifikapo Januari katikati, tutauzindua rasmi wananchi waweze kutuma malalamiko yao, ni muhimu sana kuulewa  kupitia warsha
hii, tuuelewe vizuri na kuanza kuutumia kabla ya kuuzindua, kwa sababu tutahakikisha kama kuna tatizo, mteja anafikisha kwa haraka na linafika kwa haraka  na kupata haki yake kwa haraka," amesema.

Naye Kaimu Meneja wa Kumlinda mtumiaji wa Huduma za Kifedha,  Dk. Hadija Kishimba,
amesema lengo la BoT, kuandaa warsha hiyo kwa taasisi za fedha ni kutaka watoa huduma kuuelewa mfumo, kwani wao ndiyo wanaokutana na wateja.

Aidha amewataka watumie mfumo huo kwa sababu unakwenda kusogeza huduma kwa mwananchi kwani wanataka mlalamikaje alalamike kupitia mtandao kwa njia ya kompyuta au simu janja yake.

Amesema lengo la BoT, ni kutafuta namna bora ya kutumia teknolojia kuwafikia wananchi katika kuwapa huduma, kwani jukumu la  benki hiyo ni kuongeza fedha jumuishi nchini,  hivyo  kumekuwa na changamoto  ya kuongeza imani mtu akipata tatizo apate ufumbuzi wa haraka.

Amesema kwa sasa wanapokea malalamiko kupitia matawi yao na dawati ya malamiko kupitia njia ya barua pepe, simu au kuandika barua na kufikisha hivyo, waona njia hiyo inaweza kutowafikisha  zaidi ya teknolojia.

"Tukaona tutumie mfumo kwa njia ya teknolojia, mwananchi wetu asiweze kutembea katika tawi letu kutufuata, akiwa sehemu yake ya kazi anaweza  kuandika  lalamiko lake na kuweza kusaidiwa moja kwa moja na tumefanya hivyo kwa sababu wananchi wengi wanapenda kutumia huduma za fedha lakini kutishwa na mazingira ambayo akifika anaweza asifikishe taarifa zake vizuri," amesema.

Pia, kuwasaidia kuwa na imani na sekta za fedha kwa sababu mbeleni wana malengo ufike katika mkono wa mwananchi kurahisisha upatikanaji wa haki na mwanachi akitaka kulalamika aanze na taasisi yake ya kifedha na asiporidhika atakapotumia mfumo tutamuuliza taasisi aliyotumia na kumsaidia.

"Kiutaratibu huwa tunapimwa kidunia na huwa kuna vitu wanaviangalia kwa sababu ukisema fedha jumuishi huwa tunaangalia vitu vitatu ikiwa umeizungumzia huduma, ninatumia huduma, ubora wa huduma",Amesema.

Kwa upande wake, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa benki ya NMB, Elizabeth Mhina  amesema wamefurahi BoT  kuweka mfumo kuwa  wa moja kwa moja  hivyo itawasaidia  kurahisisha kazi na kuwafikia wateja na  Watanzania kwa ujumla.

"Yapo malalamiko mengi wamekuwa wakiyapokea kikubwa ni changamoto ya elimu kwa wateja kwa mfano kuibiwa fedha katika ATM  na kadi wamekuwa wakiyapata kila siku, ni suala  la elimu kuwa wasitoe namba za siri, bado tunatoa elimu kuwafikia wateja wetu  kudhibiti wizi," amesema.

Naye mtoa huduma za fedha wa benki ya CRDB, Lugano Mponjoli amesema hatua hiyo italeta mabadiliko katika mfumo wa fedha na kutatua changamoto za wateja kwa muda mfupi ikiwemo  za kuibiwa fedha  hivyo lakini pia itasaidia namna ya kuweza kutunza taarifa zao.

UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI  KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.

UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.

THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.

THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.

JUMUIYA YA USIMAMIZI WA USAFIRI MAJINI AFRIKA ZATAKIWA KUUNGANA ILI KUIMARISHA USALAMA SEKTA YA USAFIRI MAJINI.

JUMUIYA YA USIMAMIZI WA USAFIRI MAJINI AFRIKA ZATAKIWA KUUNGANA ILI KUIMARISHA USALAMA SEKTA YA USAFIRI MAJINI.

TAASISI ZA UMMA ZAHIMIZWA KUTENGA ASILIMIA 30 YA BAJETI YA MANUNUZI KWA AJILI YA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM.

TAASISI ZA UMMA ZAHIMIZWA KUTENGA ASILIMIA 30 YA BAJETI YA MANUNUZI KWA AJILI YA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM.

NIC YAZINDUA KAMPENI YA NIC KITAA ILI KUTOA ELIMU YA BIMA KWA WANANCHI.

NIC YAZINDUA KAMPENI YA NIC KITAA ILI KUTOA ELIMU YA BIMA KWA WANANCHI.