

Katika kipindi cha kuanzia Julai 2024 hadi Machi 2025, bei ya madini ya dhahabu kwa wakia ilipanda hadi kufikia wastani wa dola za Marekani 2,655.80 ikilinganishwa na bei ya wastani wa dola za Marekani 2,078.09 katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024.
Kuongezeka kwa bei ya dhahabu kumetokana na sababu mbalimbali ikiwemo mahitaji makubwa ya madini hayo duniani kama njia ya kuhifadhi thamani ya fedha.
Hayo yameelezwa Leo Mei 02.2025 na Waziri wa Madini Mhe,Anthony Mavunde wakati akiwasilisha Makadirio ya bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Bungeni Jijini Dodoma.
Kwa kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, mwenendo wa biashara ya madini ya almasi duniani umeendelea kukabiliwa na changamoto zinazosababishwa na mdororo wa uchumi wa dunia; uwepo wa almasi zinazotengenezwa kwenye maabara (Lab-Grown Diamonds) na kupungua kwa uhitaji katika masoko makubwa yakiwemo ya China na Marekani.
Aidha, bei ya madini hayo imeshuka kutoka wastani wa dola za Marekani 206.61 kwa karati mwaka 2023/2024 na kufikia dola za Marekani 168.95 kwa karati katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025 sawa na upungufu wa asilimia 18.
Aidha takwimu zinaonesha wastani wa mauzo ulikuwa karati 281,021.99 zenye thamani ya dola za Marekani milioni 47.48 ikilinganishwa na karati 164,837.94 zenye thamani ya dola za Marekani milioni 34.06 katika kipindi kama hicho cha mwaka uliopita.
"katika kukabiliana na changamoto hii, wazalishaji wakubwa wa almasi duniani wamepunguza uzalishaji ili kuimarisha bei"
Aidha, kwa upande wa Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha biashara ya almasi kwa kuanzisha minada, maonesho, masoko na kuhamasisha uwekezaji katika uchakataji wa madini ya almasi ndani ya nchi.
Aidha Wizara ya Madini kupitia taasisi zake imeendelea kuwahamasisha wachimbaji wadogo kuanzisha vikundi katika shughuli za madini na kutunza kumbukumbu za uzalishaji na biashara za madini ikiwa ni miongoni mwa vigezo vya kuwawezesha kupata mikopo kwenye taasisi za fedha.
Katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025 jumla ya shilingi 51,422,401,572.00 zilikopeshwa kwa wachimbaji wadogo 127.
Mhe,Mavunde amesema Wizara ya Madini kupitia (STAMICO) imeendelea kuratibu shughuli za uchimbaji mdogo kwa kutoa huduma za kitaalamu kwa wachimbaji wadogo katika nyanja za utafiti, uchimbaji, uchenjuaji madini pamoja na utunzaji wa mazingira.
Sanjari na hayo katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, jumla ya wachimbaji wadogo 471 wamepatiwa mafunzo kupitia vituo vya mfano vya Katente, Lwamgasa na Itumbi ambapo mpaka sasa wachimbaji 12 wa madini wameanzisha vituo vyao baada ya kujifunza kupitia vituo hivyo.
Aidha, kupitia vituo vya mfano, huduma ya uchenjuaji mbale za dhahabu kwa wateja 41 ilitolewa ambapo dhahabu ya uzito wa kilogramu 119.57 yenye thamani ya shilingi 23,318,849,170.45 ilichenjuliwa.
"Katika kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata taarifa za jiolojia, huduma za uchorongaji kwa gharama nafuu zilitolewa kwa wachimbaji wadogo 14 katika maeneo ya Tambi–Mpwapwa, Nyawa–Bariadi, Matondo, Makongolosi na Matundasi–Chunya, Lwamgasa, Nyaruyeye, Nyakagwe na Nyamalimbe–Geita, Endabash-Karatu pamoja na Mavota–Biharamulo. Jumla ya mita 3,306.47 zimechorongwa katika maeneo hayo.Amesema Mhe,Mavunde.
EVANCE KAMENGE AJITOLEA KUSAIDIA JAMII KAGERA
SERIKALI KUTEKELEZA MFUKO WA UBUNIFU WA SAMIA “SAMIA INNOVATION FUND” WENYE THAMANI YA BIL 2.3
SERIKALI YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA WALIMU 70,657 UTEKELEZAJI MITAALA ILIYOBORESHWA, YAANZA MAPITIO SHERIA YA ELIMU
DKT. DORIYE AVISHA VYEO VYA KIJESHI MAAFISA 145 NA ASKARI 476 WA NCAA NA KUSISITIZA UCHAPAKAZI, NIDHAMU, MAADILI NA UZALENDO KATIKA ULINZI WA RASILIMALI.
WAHUKUMIWA MIAKA 20 GEREZANI KWA KUHUJUMU MRADI WA ETDCO
Ibraah Afunguka: "Nilifukuzwa Konde Gang na Harmonize"
Watu Wenye Ulemavu Waomba Kuangaliwa kwa Jicho la Kipekee Katika Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.
Sekta ya Uvuvi imetoa ajira ya Moja Kwa Moja Kwa Wavuvi 201,661
BODI YA ITHIBATI YATAMBULISHWA RASMI BUNGENI
SERIKALI Imeendelea Kujenga na Kuboresha Miundombinu ya Viwanja vya Ndege