

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja la Pangani.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Seleman Moshi Kakoso amesema kazi iliyofanywa kwenye daraja hilo lenye urefu wa meta 525 ni kubwa hivyo Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), wahakikishe daraja hilo linakamilika kwa wakati ili kukuza fursa za uwekezaji katika ushoroba wa fukwe za mikoa ya Tanga na Pwani.
Hakikisheni kasi ya ujenzi wa daraja iendane na ujenzi wa barabara ili vikamilike na kutoa huduma mara moja", amesema Kakoso.
Kamati hiyo inayoendelea na ukaguzi wa miradi ya kimkakati katika mkoa wa Tanga imekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani- Bagamoyo Km 256 ambayo ujenzi wake unaendelea.
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya ameihakikishia Kamati hiyo ya Bunge kuwa barabara ya Tanga-Pangani ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 75 itakamilika Juni mwaka huu.
" Tumejipanga kuhakikisha sehemu hii ya kwanza Tanga-Pangani inakamilika ifikapo mwezi Juni wakati daraja likitarajiwa kukamilika Disemba mwaka huu", amebainisha Naibu Waziri Kasekenya.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Mohamed Besta amesema ujenzi huo umegawanywa katika sehemu nne ili kuharakisha ujenzi wake.
Amezitaja sehemu hizo kuwa ni Tanga-Pangani km 50, daraja la Pangani meta 525 na barabara unganishi km 25.6, barabara ya Mkange-Mkwaja-Tungamaa km 95.2 na sehemu ya Mkange-Bagamoyo Makurunge km 73.25 ambayo usanifu wake umekamilika.
Kukamilika kwa barabara hii kutachochea ukuaji wa uchumi, kupunguza gharama na muda wa safari, kuwezesha kufikika kwa urahisi vivutio vya utalii na kuunganisha kwa njia fupi bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mombasa.
Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"
TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.
Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.
NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.
PPAA yawanoa wazabuni Kanda ya Kaskazini
NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.
DrKumbuka Afunguka Kuhusu Kuvunjika kwa Ndoa ya Haji Manara na Zaiylissa
Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu
Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma