

Kampeni ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia, iliyozinduliwa na Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa ni miongoni mwa kampeni zilizofanikiwa kwa kiwango cha juu, kutokana na jitihada za Serikali katika kuelimisha jamii, juu ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia na umuhimu wake katika kulinda Afya ya binaadamu na utunzaji wa mazingira, sambamba na kugawa mitungi ya gesi kwa wananchi.
Akielezea jitihada za Rais Samia, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema, Rais Dkt. Samia ameiheshimisha Tanzania katika hamasa ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia ambapo kutokana na jitihada hizo, Mashirika ya Kimataifa yameonesha nia ya kumuunga mkono ikiwemo kufanya Mkutano mkubwa wa Nishati safi Afrika hapa nchini.
“Watanzania tumuunge mkono Rais Samia katika kampeni hii na kuhakikisha tunaongoza kwenye matumizi ya Nishati Safi Barani Afrika, tunapaswa kumuunga mkono kwa sababu agenda imeanzishwa na Rais wetu, Dunia lazima iitambue Tanzania kama ambavyo imetambua na kuleta mkutano mkubwa wa Nishati Safi hapa nchini, tusiwe nyuma, tuwe mstari wa mbele,” amesema Majaliwa.
Kiongozi huyo amesema hayo Disemba 31, 2024 wakati wa Tamasha la Azimio la Kizimkazi ambalo lilienda sambamba na ugawaji wa majiko 1,000 ya gesi kupitia kampeni ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia, tukio lililofanyika katika eneo la Kilimahewa Majumbakumi, Ruangwa Mkoani Lindi.
Ametoa wito kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuibeba ajenda ya Nishati Safi ya kupikia na kuhamasisha umuhimu wa matumizi ya Nishati hiyo ikiwemo umeme, gesi na mkaa rafiki.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amesema kuwa azimio la kizimkazi linakwenda kuwa mkombozi kwa mwanamke kupata Nishati Safi ya kupikia.
Majaliwa amegawa mitungi hiyo 1000 ya gesi ambayo 800 imetolewa na Shirika la Utangaji Tanzania kupitia Bongo Fm na mitungi 200 imetolewa na Taifa gesi.
#2025Betterthanever #KAZIINAONGEA
WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WAASWA KUZINGATIA MADILI
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI
WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.
SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.
AZANIA BENKI BUNGE BONANZA LAWALETA PAMOJA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA.
MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUKUTANA KATIKA BONANZA LA KUHAMASISHA MICHEZO NA UMUHIMU WA MAZOEZI.
MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.
RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.
WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI