SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA HADI IFIKAPO 2030 ASILIMIA 80% YA WATANZANIA WANATUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Nishati

SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA HADI IFIKAPO 2030 ASILIMIA 80% YA WATANZANIA WANATUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

Naibu Waziri na Waziri wa Nishati Mhe.Doto Mashaka Biteko amesema Sekta ya nishati itaendelea kutatua changamoto zote zinazoikabili sekta hii ikiwa ni pamoja na kuhamasisha nishati safi ya kupikia pamoja na kuhakikisha asilimia 80% ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2030.

Moreen Rojas, Dodoma.
By Moreen Rojas, Dodoma.
05 Nov 2024
SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA HADI IFIKAPO 2030 ASILIMIA 80% YA WATANZANIA WANATUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

Biteko ameyasema hayo leo novemba 5 jijini Dodoma wakati  akizungumza na wadau wa nishati na madini katika Jukwaa la uziduaji 2024 Agenda iliyoandaliwa na Haki Rasilimali.

Aidha ametoa Rai kwa wadau wa mkutano huo kwamba mijadala yote itakayokuwa inajadiliwa iwe yenye tija lakini pia majadiliano hayo Serikali itayachukua na kuyafanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuambiana ukweli kuhusu umuhimu wa nishati safi ili kuhakikisha tunapata maendeleo Kwa pamoja kama nchi.

Kwa upande wake Waziri wa Madini Antony Mavunde amesema Sekta ya madini imeendelea kukua Kila siku kwani moja kati ya mkakati mkubwa ni kufanya utafiti wa kina katika eneo kubwa la asilimia 16 kwani nchi imepata manufaa ambapo Sekta ya madini imeingiza Dola za kimarekani bilioni 3.1 ambayo ni sawa na asilimia 56%.

Aidha ameongeza kuwa mwaka huu wa fedha wamejipanga kuingizia Serikali  trilioni 1 maduhuli ifikapo mwezi wa 6 mwakani kwani nchi ya Tanzania ina madini ya kutosha na madini mkakati ambapo hivi sasa wanamkakati maalum wa kuyavuna madini mkakati.

Akitoa salam za Mkoa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewashukuru haki Rasilimali Kwa kuchagua mkoa wa Dodoma kuweza kufanya mkutano wao kwani wamechagua sehemu sahihi na sehemu salama.

Aidha amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Kwa kazi kubwa anayoifanya kwenye sekta ya madini hasa kutoa upendeleo kwa mkoa huu kwani utafiti uliofanyika unaonyesha mkoa wa Dodoma unaongoza kwa kuwa na madini mengi tofauti na mikoa mingine.

"Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania nalo ni kivutio,kwani nchini, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla hakuna la namna hiyo zaidi ya Dodoma"Ameongeza Senyamule

Naye Adam Anthony Mkurugenzi Haki Rasilimali amesema anawashukuru wadau pekee na washiriki kutoka Kenya,Uganda na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo Kwa kukubali kuja kubadilishana uzoefu.

Aidha amesema jukwaa la uzinduaji limewakutanisha washiriki takribani 200 kutoka sehemu mbalimbali kuweza kujadili mambo mbalimbali ikiwemo ushiriki wa wanawake kwenye sekta ya madini na sekta ya nishati ikiwa ni sambamba na Serikali kukemea vitendo vya Rushwa.

Sanjari na hayo Mwenyekiti wa Bodi Haki Rasilimali Jimmy Luhende ameiomba Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine kuangalia  namna bora na Salama kimazingira Kwa wanaotumia zebaki,ikiwa ni pamoja na  kutafuta namna mbadala ya kunasa madini bila kupata madhara yoyote.

"Serikali ijaribu kuwaangalia akina mama watenge maeneo ya leseni waweze kuwapatia vikundi vya kina mama kwani wanatumia nguvu kubwa kipato kidogo mfano kuponda mawe na kusafisha  madini, hivyo Serikali iangalie namna bora ya kuwafikia kina mama ili waweze kujikwamua kiuchumi"Amesema Mchimbaji mdogo wa madini Ndugu.Amos Juma.

JAMII YAASWA KUTUMIA NISHATI SAFI ILI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MHE.RAIS

JAMII YAASWA KUTUMIA NISHATI SAFI ILI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MHE.RAIS

REA KUSHIRIKIANA NA NJOMBE KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI ZAIDI YA 13,000

REA KUSHIRIKIANA NA NJOMBE KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI ZAIDI YA 13,000

BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT

BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT

REA YASAINI MIKATABA YA KUPELEKA UMEME KWENYE VITONGOJI 3,060 KOTE NCHINI

REA YASAINI MIKATABA YA KUPELEKA UMEME KWENYE VITONGOJI 3,060 KOTE NCHINI

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAAHIDI KUUPA MSUKUMO MRADI WA EACOP

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAAHIDI KUUPA MSUKUMO MRADI WA EACOP