WANNE WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

WANNE WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuhusika katika matukio manne ya mauaji yaliyo tokea kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti katika jiji la Dodoma.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
27 Sep 2024
WANNE WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

Hayo yameelezwa hii leo na Kamanda wa Polisi jijini Dodoma SACP George Katabazi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa hali ya usalama jijini hapa.

Aidha amesema kuwa watuhumiwa hao wanne ni pamoja na Paulo Daudi Mwaluko mwenye miaka 22,mkulima na mkazi wa mtumba,Isack Richard mwenye miaka 24,mkulima mkazi wa mtumba,Ernest Richard mwenye miaka 18,mkulima  mkazi wa Mtumba pamoja na Silvanus Shotoo mwenye miaka 21,mkulima na Mkazi wa mtumba.

Aidha ameongeza kuwa tukio la kwanza ni tukio lililotokea Julai 01,2024 katika eneo la Mahomanyika Nzuguni ambapo waliuawa mabinti wawili usiku ndani ya Grosari waliokuwa wakifanya kazi kisha miili yao kuchomwa na moto.

"Tukio la pili lilitokea Agosti 28,2024 eneo la Mbuyuni Kizota ambapo aliuawa mwanaume mmoja na mke wake alijeruhiwa na watoto wake watatu kisha godoro walilokuwa wamelalia kuchomwa moto ili waungue"Amesema

Aidha tukio la tatu ni ambalo limetokea Septemba 6,2024 huko eneo la Mkonze ambapo mama mmoja na mtoto wake waliuawa.

" Tukio la nne lilitokea Septemba 16,2024 huko katika mtaa wa Segu Bwawani Nala ambapo mabinti watatu waliuawa na kuchomwa moto na mama mwenye nyumba alijeruhiwa"

Sanjari na hayo Uchunguzi umebaini kuwa katika matukio yote hayo watuhumiwa wakishapiga kwa kitu kizito wanaowakuta kwenye nyumba waliovamia huwafanyia vitendo vya udhalilishaji kisha kuchoma moto ili ionekane ni shoti ya umeme imetokea ambapo uchunguzi zaidi unakamilishwa ili hatua zingine za kisheria zifuate.

Aidha Jeshi la Polisi linapenda kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano wao uliofanikisha kukamatwa kwa mtandao huu wa mauaji.

TRENI YA MCHONGOKO KUSIMAMA KWA SAA SITA NI HUJUMA:TRC

TRENI YA MCHONGOKO KUSIMAMA KWA SAA SITA NI HUJUMA:TRC

SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA SERA YA UTEKELEZAJI YA TEHAMA.

SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA SERA YA UTEKELEZAJI YA TEHAMA.

SOKO SWAHILI MARKET KUJA NA FURSA KWA WAJASILIAMALI WADOGO.

SOKO SWAHILI MARKET KUJA NA FURSA KWA WAJASILIAMALI WADOGO.

RAIS DKT.SAMIA AMETOA MSISITIZO KWA WATANZANIA KUHAKIKISHA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA UNAMALIZIKA BILA KULITIA DOA TAIFA.

RAIS DKT.SAMIA AMETOA MSISITIZO KWA WATANZANIA KUHAKIKISHA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA UNAMALIZIKA BILA KULITIA DOA TAIFA.

Wasichana waaswa kutumia mitandao kwa manufaa

Wasichana waaswa kutumia mitandao kwa manufaa