Dodoma.JESHI la kujenga Taifa nchini JKT limesema linatoa mafunzo kwa Vijana wa kitanzania kwajili ya kujiajiri lakini halitoi ajira.
Kaimu Mkuu wa Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa JKT Juma Mrai ameyaeleza hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kutoa wito kwa Vijana wa Kitanzania kujiunga na mafunzo ya kujitolea Kwa Mwaka 2024.Aidha Kanali Mrai ametoa wito kwa Wananchi kujihadhari na matapeli ambao wamekuwa wakitumia fursa hiyo kudanganya watu kuwa Jeshi la JKT linatoa ajira na kuwatapeli wananchi.Aidha Usaili wa vijana hao kujiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa kwa kujitolea utaanza tarehe 01 oktoba,2024 kwa mikoa yote Tanzania bara na visiwani,Vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya Jeshi kuanzia tarehe 01Novemba,2024 hadi 03 Novemba 2024.
"Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo,unaratibiwa na ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya ambako mwombaji anaishi"Aidha Jeshi la kujenga Taifa linapenda kuwataarifu Vijana watakaopata fursa hiyo kuwa Jeshi la kujenga Taifa kuwa halitoi ajira,pia halihusiki kuwatafutia ajira katika Asasi,Vyombo vya Ulinzi na Usalama na mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyo ya kiserikali,bali hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza mkataba wao na Jeshi la kujenga taifa.
" Sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo yanapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz"
Sanjari na hayo Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawakaribisha vijana wote watakaopata fursa hiyo kujiunga na vijana wenzao ili kujengewa Uzalendo,Umoja wa kitaifa,Ukakamavu,Kufundishwa stadi za kazi,Stadi za Maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa lao.
MABADILIKO YA TABIA YA NCHI CHANZO CHA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA MAZAO
RAIS DKT.SAMIA ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI KUZINDUA RASMI MFUKO WA MKOPO KWA AJILI YA KUSAIDIA BUNIFU.
TRENI YA MCHONGOKO KUSIMAMA KWA SAA SITA NI HUJUMA:TRC
SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA HADI IFIKAPO 2030 ASILIMIA 80% YA WATANZANIA WANATUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.
PROF.MALEBO:TANZANIA YAFAFANUA UMOJA WA MATAIFA KUWA HAINA ARDHI YA MAKABILA
MABADILIKO YA TABIA YA NCHI CHANZO CHA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA MAZAO
SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA HADI IFIKAPO 2030 ASILIMIA 80% YA WATANZANIA WANATUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.
TRENI YA MCHONGOKO KUSIMAMA KWA SAA SITA NI HUJUMA:TRC
RAIS DKT.SAMIA ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI KUZINDUA RASMI MFUKO WA MKOPO KWA AJILI YA KUSAIDIA BUNIFU.