

Muwakilishi wa wanawake mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Sophia Mwakagende amelipongeza shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kwa maboresho makubwa waliyoyafanya katika kuhudumia umma hasa katika ulimwengu wa kidigitali.
Pongezi hizo amezitoa leo Agosti 06,2024 Jijini Dodoma mara baada ya kutembelea banda la Shirika hilo lililopo kwenye maonesho ya Nanenane Nzuguni.
Amesema shirika limefanya maboresho makubwa kuendana na wakati uliopo sasa kwani wanawafikishia huduma wananchi mpaka kwenye makazi yao kwa kupitia huduma yao ya fiber Mlangoni.
"Niipongeze sana Serikali chini ya usimamizi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia shirika hili la TCCL Kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika tumeona sasa mtandao wa interneti unapatikana kila sehemu na ukizingatia sasa hivi Dunia ipo kiganjani",Amesema.
Amesema maboresho yaliyoafanyika wao kama jicho la pili la serikali wameridhishwa na kuahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha mtandao wa TTCL unafika mbali zaidi.
Ameongeza kuwa ufanyaji wa biashara kwa sasa unategemea zaidi mtandao lakini pia kuanza kwa treni ya umeme SGR kunategemea zaidi mtandao haswa katika ukataji wa treni ili kupunguza msululu kwenye madirisha ya kukatia tiketi.
Sambamba na hayo Mwakagenda ametoa rai kwa shirika hilo kuhakikisha wanafukisha huduma ya internet kwa shule za sekondari zilizopo vjijini ili kuwasaidia kujifunza.
"Niwaombe TTCL kupeleka huduma hii kwa shule za sekondari zilizopo vijijini wapate huduma hii kwenye maktaba zao na maabara zao ili waweze kujifunza kwa vitendo",Ameongeza Mwakagenda.
Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"
TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.
Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.
NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.
NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.
Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu
Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma
WADAU WA UNUNUZI WAASWA KUZINGATIA MAADILI KAZINI
Watumishi wa Bodi ya maziwa waaswa kuzingatia weledi katika kazi zao.