DIB YAJA NA MKAKATI WA MIAKA MITANO UTOAJI WA ELIMU KWA UMMA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

DIB YAJA NA MKAKATI WA MIAKA MITANO UTOAJI WA ELIMU KWA UMMA.

Bodi ya Bima ya Amana(DIB) imesema imeweka mkakati wa miaka mitano wa utoaji wa elimu kwa umma ili kuhakikisha kila mwananchi anafahamu usalama wa fedha zake alizoziweka benki kama akiba.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
06 Aug 2024
DIB YAJA NA MKAKATI WA MIAKA MITANO UTOAJI WA ELIMU KWA UMMA.

BODI ya Bima ya Amana(DIB) imesema imeweka mkakati wa miaka mitano wa utoaji wa elimu kwa umma ili kuhakikisha kila mwananchi anafahamu usalama wa fedha zake alizoziweka benki kama akiba.

Pia inawakaribisha wananchi walioshiriki waonesho ya wakulima Nanenane katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma kufika kwenye banda la bodi hiyo ili kupata elimu ya usalama wa fedha zao.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo Agosti 5,2024 Meneja Uendeshaji DIB Nkano Magina amesema wapo kwenye maonesho hayo ili kutoa elimu kwa wananchi na  wamejipanga kuhakikisha elimu hiyo inatolewa kwa kila mwananchi.

"Tunawakaribisha wananchi kwenye banda letu ili wapate  elimu kuhusu usalama wa fedha zao walizoweka benki kama akiba",Amesema.

Amesema DIB katika mpango wake wa miaka mitano wameweka mkakati wa kutoa elimu kwa umma ambapo mpaka kufikia 2026/2027 wanampango wa kuwafikia wateja wa benki kwa asilimia 30 na umma wa watanzania asilimia 20.

Aidha amesema kuwa majukumu DIB ni pamoja na kusimamia mfuko wa bima ya amana ambao unachangiwa na mabenki yote yaliyopewa leseni na benki Kuu ya kufanya biashara hiyo.

"Pale benki inapofugwa na benki kuu na kuwekwa chini ya ufilisi jukumu la bodi ya bima ya amana ni kulipa fidia ya bima ya amana ili wateja waliokuwa wanahudumiwa na hiyo benki wasipoteze pesa zao",Amesema.

Amesema kwa sasa kiwango cha juu cha fidia ya bima ya amana kwa wateja wa benki yoyote ambayo wanaleseni ya BoT ikifilisiwa  ni kuanzia shilingi moja mpaka milion 7.5 ambapo kwa kiwango hiko wamewafikia wateja kwa asilimia 99 ambao ni benki na taasisi za fedha hapa nchini

Aidha ameongeza kuwa mpaka sasa benki 9 za zamani zimefilisiwa na hatua wamefikia kwenye hatua nzuri ya kuzifidia.

Aidha amesema maoni ya wananchi wengi waliopita kwenye banda lao ni kutaka Saccos na vicoba navyo nianzishiwa bima ya amana kama ilivyo kwenye mabenki.

DIB ilianzishwa kwa sheria ya benki na taasisi za fedha ya mwaka 1991ambayo iliuhishwa mwaka 2006.

TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini

TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini

VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI

VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI

BRELA YAWATAKA WASANIFU MAJENGO NA WAJASIRIAMALI KUTUMIA VIZURI BUNIFU ZAO.

BRELA YAWATAKA WASANIFU MAJENGO NA WAJASIRIAMALI KUTUMIA VIZURI BUNIFU ZAO.

MCHENGERWA AZINDUA MFUMO WA KADI JANJA ZA MWENDOKASI AWATAKA DART NA UDART KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAGARI.

MCHENGERWA AZINDUA MFUMO WA KADI JANJA ZA MWENDOKASI AWATAKA DART NA UDART KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAGARI.

MRAJISI VYAMA VYA USHIRIKA AGUSWA NA HUDUMA YA MALIPO KWA MKUPUO YA TTCL.

MRAJISI VYAMA VYA USHIRIKA AGUSWA NA HUDUMA YA MALIPO KWA MKUPUO YA TTCL.