MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Taifa ya Ushindani (FCC) William Urio amewataka wananchi, wakulima na wafugaji Kufika katika viwanja vya Maonesho ya Nanenane kujifunza namna bora ya tume ya Ushindani inavyofanya kazi hasa katika suala zima la kumlinda mlaji.
MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Taifa ya Ushindani (FCC) William Urio amewataka wananchi, wakulima na wafugaji Kufika katika viwanja vya Maonesho ya Nanenane kujifunza namna bora ya tume ya Ushindani inavyofanya kazi hasa katika suala zima la kumlinda mlaji.
Pia, amewataka kuhakikisha wanatumia pembejeo zenye ubora ili waweze kupata mazao yenye bora.
Hayo ameyasema leo Agosti 5,2024 kwenye Maonesho ya wakulima na wafugaji yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Nanenane-Nzuguni Jijini Dodoma
Amesema Tume ya Ushindani ndicho chombo kinashughulikia masuala ya ushindani wa kibiashara, ina jukumu muhimu la kutoa ushauri kwa kampuni zinazoshindana katika soko ikiwemo kujitambulisha kwa Soko,kulijua soko vizuri na mahitaji ya wateja.
" FCC tunajukumu la kuhakikisha mfanya biashara anatambua nafasi yake katika soko ili kuboresha bidhaa na upekee, ili kuwa na tija mfanyabiashara anapaswa kujitofautisha kupitia bidhaa , tafuta njia za kutofautisha bidhaa zako zile za washindani hii itaboresha ubora, kuongeza vipengele vya kipekee, au kutoa huduma bora kwa wateja,"amesisitiza mkurugenzi huyo
Mkurugenzi huyo wa FCC ameongeza kuwa kila mfanyabiashara anapaswa kuhakikisha bidhaa zake zinakidhi viwango vya ubora vinavyotambulika na vya kisheria na kufafanua kuwa ubora wa bidhaa unaweza kuwa kipande muhimu katika ushindani.
"Kwenye kilimo kuna suala zima la pembejeo hivyo ni wakati sahihi wa wakulima kuja na kupata elimu ya ufahamu ya pembejeo feki lakini pia kwa upande wa wavuvi wanahitaji elimu wanapataje nyavu sahihi bila kusahau vifungashio viwe venye kukidhi viwango, "Amesema
Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa,amewataka Wafanyabiashara na wakulima kwa ujumla kujiandikisha kwenye daftari la Mpiga kura ili kupata nafasi ya kuwachagua Viongozi wenye maono na fursa zinazowahusu.
Ameeleza kuwa Viongozi hao wanapaswa kuwa na uelewa mzuri wa mahitaji ya wafanyabiashara na sera zinazohitajika ili kuboresha kilimo na fursa zake
"Viongozi bora ni wale wenye mipango thabiti na mikakati ya maendeleo ya kilimo na kuweza kujumuisha mipango ya kuboresha miundombinu, masoko, na upatikanaji wa huduma za kilimo, " Amesema.
"Niwaombe wafanyabiashara,wakulima,wavuvi na wafugaji mchague viongozi wenye uwezo wa Kuleta mabadiliko Viongozi wenye mtandao mzuri na uhusiano na wanaweza kusaidia kufanikisha ushirikiano wa kibiashara, kupata ruzuku, na rasilimali nyingine za maendeleo,viongozi wanapaswa kuwa na uwezo wa kusimamia na kuboresha huduma za kibiashara na kilimo kwa kujumuisha usimamizi wa ardhi, maji, na miundombinu ya kilimo, "amesema Mkurugenzi huyo
DKT. BITEKO ataka TANESCO kuongeza kasi utekelezaji miradi ya umeme wa gridi
Ndaisaba azidi kumwaga Fedha katika sekta ya Michezo Wilayani Ngara
"Hatutawavumilia wanaochochea Machafuko Nchini" Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
VIJANA NDIO WALINZI WA NCHI HII: MEJA JENERALI RAJABU MABELE
BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT
VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja