Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imedhamiria kuwawezesha vijana katika sekta ya kilimo kwa kuwapatia dhana mbalimbali ikiwemo matrekta ili wakulima waweze kulima kwa tija huku ikiwataka wananchi kujitokeza katika maonyesho ya nanenane kujionea teknolojia za kisasa ambazo zitawasaidia.
Kauli hiyo ya serikali ameitoa Naibu Waziri wa kilimo,David Silinde katika viwanja vya nanenane Jijini Dodoma mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali na kujionea teknolojia za kilimo.
"Kama serikali tumejipanga katika kuhakikisha vijana wanapata uelewa kuhusu kilimo na tayari tushatoa maelekezo kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwajili ya vijana ili Taifa letu la Tanzania lijitosheleze na mazao ya kilimo". Amesema Silinde
Aidha amesema serikali imejipanga hadi ifikapo mwaka 2030 Itakuwa itimiza lengo lake la kuwa na Matrekta elfu10 ili kumfikia kila mkulima ili aweze kulima kwa tija huku akiwataka wananchi kujitokeza katika maonyesho ya nane nane kujionea teknolojia za kisasa ambazo zitawasaidia.
"niwapongeze Wenzetu wa Kampuni ya Pass Leasing kwa kutoa trekta na zana mbalimbali za kulimia kwa wakulima wa Tanzania, leo mmepokea nyie wa kutokea Chemba na Kongwa lakini Mpango wa serikali ifikapo 2030 serikali itakuwa imetimiza kugawa trekta elfu 10 kwa wakulima wetu", amesema
"Makubaliano haya yanalenga kuhakikisha wakulima na wajasiriamali wanapata bidhaa bora, na huduma baada ya mauzo ikiwemo mafunzo na huduma za utengenezaji wa zana,hadi kufikia sasa kwa kushirikiana na kampuni hii tumeweza kwa pamoja kutoa zana mbalimbali zaidi ya 350, ambazo zipo kwenye ubora wa juu na wakulima wanafurahia huduma zao na Kampuni hii inahudumia wateja nchi nzima kupitia matawi yake yaliyopo Dar es salaam (makao makuu), Melela, Mbeya, Igurusi, Kahama, Mwanza, Sumbawanga na Babati",
Kiukweli nawashauri wananchi wenzangu waje wajionee mambo mazuri yanayopatikana hapa 88 kwenye mabanda mabalimbali haswa wafugaji wenzangu njooni mjifunze namna ya kufuga kisasa yaani ufugaji wenye tija kwa sababu kunawataalamu wabobezi wa masuala haya watakuelekeza namna bora ya kufuga kisasa na kunufaika na kuacha mazoea ya ufugaji holela usiokuwa na tija" Amesema Semeni Kassim Mkazi wa wilaya ya Kongwa.
DKT. BITEKO ataka TANESCO kuongeza kasi utekelezaji miradi ya umeme wa gridi
Ndaisaba azidi kumwaga Fedha katika sekta ya Michezo Wilayani Ngara
"Hatutawavumilia wanaochochea Machafuko Nchini" Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
VIJANA NDIO WALINZI WA NCHI HII: MEJA JENERALI RAJABU MABELE
BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT
VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja