

Mkurugenzi wa kampuni ya Namburi Agricultural Company ambao ni wazalishaji wa mbegu bora Dkt Mary Mgonja amewataka wakulima nchini kutumia mbegu zinazozalishwa nchini ambazo zinaviwango na zinahimili ardhi aina zote.
MKURUGENZI wa kampuni ya Namburi Agricultural Company ambao ni wazalishaji wa mbegu bora Dkt Mary Mgonja amewataka wakulima nchini kutumia mbegu zinazozalishwa nchini ambazo zinaviwango na zinahimili ardhi aina zote ikiwemo ukame.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Augost 2,2024 kwenye maonesho ya Kimataifa ya wakulima Nanenane Mkoani Dodoma amesema kampuni yao imekuwa ikizalisha mbegu zenye ubora lakini pia zinahimili mpaka kwenye ukame.
"Hapo sisi tunambegu mpaka zinazohimili kwenye ukame mbapo mkulima wa maeneo hayo anaweza kuzitumia na akafanikiwa kuvuna vizuri na kufanyabiashara",Amesema Dkt Mgonja.
Aidha ameipingeza Wizara ya kilimo kwa kushirikiana na Tosci kwa kuitangaza nchi lakini pia kuzuia uuzaji wa mbegu bandio.
"Nitoe rai kwa wakulima pia kuwa makini wakati wa kununua mbegu kuhakikisha mbegu hizo zina alama ya Tosci",Amesema.
Ameongeza kampuni ya Mamburi inafanya shughuli zake za uchakataji na uzalishaji katika mkoa wa Songwe lakini wanasambaza mbegu zao kwenye maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha kila mkulima anapata mbegu hizo.
Sambamba na hayo Dkt Mgonja amewata wastaafu kutumia muda huo wa kuingia kwenye kilimo ili kuendelea kufanyakazi na kujiimarisha kiafya na kiuchumi pia.
Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"
TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.
Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.
NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.
NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.
Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu
Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma
WADAU WA UNUNUZI WAASWA KUZINGATIA MAADILI KAZINI
Watumishi wa Bodi ya maziwa waaswa kuzingatia weledi katika kazi zao.