BALOZI NCHIMBI APOKEA TAARIFA UTEKELEZAJI ILANI MCHINGA, AMPONGEZA MBUNGE MAMA SALMA KIKWETE KWA KAZI NZURI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

BALOZI NCHIMBI APOKEA TAARIFA UTEKELEZAJI ILANI MCHINGA, AMPONGEZA MBUNGE MAMA SALMA KIKWETE KWA KAZI NZURI.

"Niseme nimeisikiliza taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, tena kwa umakini sana kwa niaba ya CCM nakupongeza wewe na viongozi wenzako kwa kazi kubwa unayofanya. Umetembelea kata zote na vijiji vyote. Umetumia hadi bodaboda na bajaji kuwafikia wananchi wa Jimbo la Mchinga, unaguswa na changamoto za wananchi wenzako wa Mchinga na unapambana kutatua kero zao kwa kuzisemea Bungeni na kuwaomba mawaziri kufika huku wao wenyewe.”

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
31 Jul 2024

“Wakati wa natazama ile video ya uwasilishaji wa taarifa hiyo ya utekelezaji wa ilani, kuna mama mmoja amesema hakutegemea kwa hadhi yako ulivyo, kwamba ungeweza kulizunguka jimbo zima la Mchinga. Mimi pamoja na wenzangu Wajumbe wa Sekretarieti tumefurahishwa sana ya utekelezaji huu mzuri wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi 2020/2025, ndani ya miaka hii mitatu. Tunakutakia kila la heri katika kumalizia hayo mengine yaliyobakia katika kukamilisha Ilani ya 2020 - 2025.”

Naye Mbunge wa Jimbo la Mchinga Salma Kikwete wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/2025, amepongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya  nchini pamoja na Jimbo la Mchinga, ambapo hadi sasa ambapo takriban Sh. 18.4 bilioni zimetumika katika Sekta ya Elimu ikiwemo kujengwa Shule ya Wasichana ya Mkoa wa Lindi Mchepuo wa Sayansi, iliyojengwa katika Kijiji cha Kilangala huku uboreshaji wa huduma za afya ukifanyika kwa mafanikio makubwa na umeme tayari umefika katika vijiji vyote jimbo zima, sasa unaanza kuunganishwa kwenye vitongoji.

Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, Mama Salma Kikwete amekabidhi pikipiki kwa Polisi Jamii wa Jimbo la Mchinga na shule za sekondari katika kata zote za jimbo hilo.

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI

WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM  KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.

WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.

SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.

SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.

WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.

WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.

RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.

RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.