Dodoma.Kuelekea Uzinduzi wa treni ya Reli ya kisasa(SGR) wananchi na wakazi wa Dodoma waaswa kuchangamkia fursa za kiuchumi.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi katika Stesheni ya Reli ya Kisasa jijini hapa ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua treni hiyo tarehe 1 Agosti 2024 ikitokea Dar es Salaam hadi Dodoma.
Aidha ameongeza kuwa wakazi wa Dodoma kwa sasa wanaweza kupeleka zabibu na biashara zingine Dar es Salaam na kurudi na hela kwa wakati jambo ambalo hapo nyuma kabla ya kutengenezwa kwa Reli ya kisasa walikuwa wanatumia muda mwingi bila mafanikio, hivyo hii ni fursa kwa wakazi wa Dodoma kuchangamka katika kujiendeleza kiuchumi.
"Kama mnavyojua Dodoma ni mkoa wa kimkakati na ni sehemu ambayo iko katikati ya nchi hivyo ni rahisi kwa kila mmoja kuweza kufika na kuangalia fursa zinazopatikana katika mkoa huu,hivyo ningewaomba wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa kwa kuweza kuchukua fremu zinazopatikana katika stesheni hii kwani mheshimiwa Rais anawapenda sana wakazi wa jiji hili na anaendelea kuifaharisha Dodoma kama makao makuu ya Nchi" Amesema Senyamule.
Aidha amewaomba wakazi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi ili kuweza kumpokea Mhe. Rais na kuweza kumpongeza kwa kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi kwani yale yaliyokuwa yanaongelewa kwamba hayawezekani sasa yanawezekana kwa vitendo.
Sanjari na hayo ametoa viakisi mwanga kwa madereva bodaboda na bajaji wanaofanya kazi katika Stesheni hiyo na kuwasihi kuzingatia usafi pamoja na uaminifu kwa wateja ili Dodoma iwe na sifa nzuriii kwa wageni wanaongia jijini hapa.
"Niwasihi vijana wangu muhakikishe mnakuwa wasafi lakini pia uaminifu kwani kupitia uaminifu jiji hili litakuwa na sifa nzurii,sio unambeba abiria alafu unamuibia tena sio sifa nzuriii lakini pia niwasihi suala la usafi ipende kazi yako hakikisha unakuwa nadhifu,lakini pia tunawaangalia nyinyi kama mabalozi wa kutangaza jiji hili kwa mgeni anayeingia kwa mara ya kwanza bila kusahau kuwa na bei elekezi kwa wateja sio huyu unamwambia elfu 20 mwingine elfu 5 unapoteza uaminifu jambo ambalo sio zuri na linakufanya unakuwa na sifa mbaya kwa jamii" Amesisitiza Senyamule
Kwa upande wake katibu wa Umoja wa madereva pikipiki na bajaji Chacha Marwa akiongea kwa niaba ya madereva hao amesema kuwa anamshukuru Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kujenga Stesheni na treni ya Reli ya kisasa (SGR) kwani itawasaidia kuweza kiwainua kiuchumi kwa kuweza kuwapokea wageni mbalimbali watakao kuwa wanaingia jijini hapa na kuwasihi wananchi wa Dodoma kuendelea kumsapoti Rais na kumuunga mkono katika kila anachikifanya kwa Maendeleo ya taifa hili.
Aidha madereva hao wameeleza furaha yao juu ya kukamilima kwa mradi huo mkubwa kwa nchi yetu na namna utakavyochangia kuinua uchumi wa Taifa, wafanyabiashara na mwananchi mmoja mmoja kwa kuokoa muda katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku za kiuchumi.
DKT. BITEKO ataka TANESCO kuongeza kasi utekelezaji miradi ya umeme wa gridi
Ndaisaba azidi kumwaga Fedha katika sekta ya Michezo Wilayani Ngara
"Hatutawavumilia wanaochochea Machafuko Nchini" Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
VIJANA NDIO WALINZI WA NCHI HII: MEJA JENERALI RAJABU MABELE
BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT
VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja