PPAA YATOA RAI KWA WAZABUNI WASIORIDHIKA NA MCHAKO WA UNUNUZI WA UMMA KUKATA RUFAA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

PPAA YATOA RAI KWA WAZABUNI WASIORIDHIKA NA MCHAKO WA UNUNUZI WA UMMA KUKATA RUFAA.

WAZABUNI wanaoomba zabuni za umma na kupata changamoto au kutoridhika na michakato ya ununuzi wa umma wametakiwa kuwasilisha malalamiko yao katika chombo cha Mamlaka ya Rufani za Zabuni za Umma (PPAA),ili kupata haki zao.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
11 Jul 2024
PPAA YATOA RAI KWA WAZABUNI WASIORIDHIKA NA MCHAKO WA UNUNUZI WA UMMA KUKATA RUFAA.

WAZABUNI wanaoomba zabuni za umma na kupata changamoto  au kutoridhika na michakato ya ununuzi wa umma wametakiwa kuwasilisha malalamiko yao katika chombo cha  Mamlaka ya Rufani za Zabuni za Umma (PPAA),ili  kupata haki zao.

Akizungumza katika banda la PPAA kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Katibu Mtendaji  wa PPAA, James Sando amesema chombo hicho kipo kwa ajili ya kusikiliza na  na kutoa suluhu ya malalamiko ya wazabuni itokanayo na michakato ya ununuzi wa umma.

Amesema wamepokea malalamiko yote kuhusu zabuni za umma,wanachofanya ni kusikiliza na kuyatafutia ufumbuzi na mengi wameyamaliza na haki imetendeka.

Amesema katika maonesho hayo wametembelewa na watu wengi waliopewa elimu na wengine kuelimishwa utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yao na kusema bado elimu inahitajika kwa wananchi wengi kufahamu mifumo ya kufuata endapo wana malalamiko.

Vilevile amesema kwa sasa wazabuni wote wanaoomba zabuni za ununuzi wa umma ni lazima watumie mfumo mpya wa kielektroniki wa manunuzi ya Umma ( NeST) kama sheria inavyotaka baada ya kuwasilisha maombi yake hufanyiwa kazi na kupata majibu.

Sando amesema mfumo huo ni rafiki na rahisi kwa sababu umerahisisha utoaji huduma kwa wazabuni badala ya kuwasilisha zabuni zao ana kwa ana sasa wanawasilisha kwa mtandao na hiyo inapunguza gharama na kuokoa muda.

Pia amesema kwa sasa PPAA inakamilisha kanuni mpya za rufani za mwaka 2024.

PPAA yatoa elimu matumizi ya Moduli Wiki ya Utumishi wa Umma

PPAA yatoa elimu matumizi ya Moduli Wiki ya Utumishi wa Umma

BRELA YAWEKA KAMBI KARIAKOO KUTOA HUDUMA YA KLINIKI YA BIASHARA KWA WAFANYABIASHARA

BRELA YAWEKA KAMBI KARIAKOO KUTOA HUDUMA YA KLINIKI YA BIASHARA KWA WAFANYABIASHARA

Sekta ya Madini Imechangia Katika Fedha Za Kigeni Hadi Kufikia Dola Bilioni 3.55

Sekta ya Madini Imechangia Katika Fedha Za Kigeni Hadi Kufikia Dola Bilioni 3.55

Sekta ya Uchukuzi Yachangia Dola za Marekani Bilioni 2.48

Sekta ya Uchukuzi Yachangia Dola za Marekani Bilioni 2.48

Mauzo Katika Soko la Jumuiya EAC Yameongezeka Hadi Kufikia Dola za Marekani Milioni 1,163.8

Mauzo Katika Soko la Jumuiya EAC Yameongezeka Hadi Kufikia Dola za Marekani Milioni 1,163.8