DKT.MPANGO ATAKA MSUKUMO UTOLEWE KWA VIJIJI NA VITONGOJI VISIVYO NA UMEME | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

DKT.MPANGO ATAKA MSUKUMO UTOLEWE KWA VIJIJI NA VITONGOJI VISIVYO NA UMEME

Makamu wa Rais, Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango ambaye yupo katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Kigoma, ameiagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa inatoa msukumo wa upatikanaji umeme kwa vijiji na vitongoji ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo.

Mwandishi Wetu-Kigoma
By Mwandishi Wetu-Kigoma
10 Jul 2024
DKT.MPANGO ATAKA MSUKUMO UTOLEWE KWA VIJIJI NA VITONGOJI VISIVYO NA UMEME

Dkt Mpango ameyasema hayo Julai 9, 2024, wakati akikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali mkoani Kigoma ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani humo.

Akiwa katika Kata ya Kalinzi na Mnanila Jimbo la Buhigwe, Dkt. Mpango alisema kuwa, changamoto za umeme kwa sasa zinashughulikiwa vizuri ambapo  ameipongeza Wizara ya Nishati na watendaji kwa ujumla kwa kazi nzuri wanayofanya kwenye utekelezaji na usimamizi wa miradi ya Sekta ya Nishati.

Akijibu hoja mbalimbali wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, aliwaagiza TANESCO na REA kuhakikisha vijiji 5 vilivyokosa umeme kwenye Kata ya Kalinzi vinapatiwa umeme kwa kuanza na vijiji 3 ambavyo wakandarasi wako kwenye eneo la mradi huku vifaa vikiwa tayari vimeshapelekwa.

Amevitaja vijiji hivyo vitatu kuwa ni Bugamba, Kigadye, na Kiziba ambapo alieleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ilichelewa kwa sababu ya mvua kubwa na Ziwa Tanganyika  kujaa ila kwa sasa utekelezaji wake unakwenda kutekelezwa.

‘’ Niwahakikishie wananchi wa Kalinzi na maeneo yote yenye changamoto ya umeme tunakwenda kuwafikia na miradi inakwenda kuanza ikiwemo miradi ya vitongoji, ujazilizi na  vijiji miji."’ Alisema Mhe. Kapinga.

Aliongeza kuwa, vitongoji 15 vya kata hiyo vinakwenda kupatiwa umeme na kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 vitongoji 4,000 vimetengewa fedha nchini ambapo wananchi wa Kalinzi pia ni wanufaika.

Kapinga alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Buhigwe kwa ufuatiliaji mzuri wa miradi na kuahidi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati iko imara kuhakikisha wananchi wanapata umeme.

Akiwa kata ya Mnanila,  Mhe. Kapinga aliwahakikishia wananchi kuwa vitongoji 107 vya jimbo la Buhigwe na Kata ya Mnanilwa ambavyo bado havijapatiwa umeme vitapatiwa na tayari wakandarasi wameanza utekelezaji wa miradi hiyo  chini ya wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Makamu wa Rais katika ziara hiyo  aliongozana na Mawaziri mbalimbali na Naibu Mawaziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, TAMISEMi, Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Maji, Wabunge kutoka Mkoa wa Kigoma pamoja na viongozi wa Wizara ya Nishati wakiongozwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Innocent Luoga.

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI

WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM  KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.

WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.

SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.

SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.

WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.

WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.

RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.

RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.