ENG.MRAMBA ;TPDC SHIRIKISHENI SEKTA BINAFSI USAMBAZAJI GESI ASILIA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

ENG.MRAMBA ;TPDC SHIRIKISHENI SEKTA BINAFSI USAMBAZAJI GESI ASILIA.

KATIBU Mkuu wizara ya Nishati Felician Mramba amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi TPDC kwa uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia huku akiwataka kuongeza kasi ya usambazaji wa gesi hiyo kwa kushirikisha sekta binafsi.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
09 Jul 2024
ENG.MRAMBA ;TPDC SHIRIKISHENI SEKTA BINAFSI USAMBAZAJI GESI ASILIA.

KATIBU Mkuu wizara ya Nishati Felician Mramba amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi TPDC kwa uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia huku akiwataka kuongeza kasi ya usambazaji wa gesi hiyo kwa kushirikisha sekta binafsi.

Pongezi hizo amezitoa mara baada ya kutembelea banda la TPDC lilipo kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa leo Julai 9,2024 

Amesema kufuatia na kuendelea na kukua kwa uchumi TPDC wanapaswa kuzishirikisha Sekta binafsi ili kuharakisha usambazaji wa gesi ya kupika majumbani unaenda kwa haraka.

"Kama tukiendelea kuwategemea TPDC peke yake katika usambazaji wa gesi ya kupikia tutachelewa sana kufikia malengo hivyo tunapaswa kuzishirikisha sekta binafsi ili kuharakisha mradi huu",Amesema.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa vituo vya kujazia gesi kwenye magari amesema serikali imejipanga kuongeza vituo nchi nzima ili kuhakikisha huduma inamfikia kila mwananchi.

"Tumejipanga kuhakikisha hivi vituo vya kujazia gesi vinaongezeka na kuwa vingi zaidi lakini pia tunampango wa kuanza kutumia magari maalumu yatakayotumika kama vituo vya kujazia gesi kwani malengo yetu mpaka kufikia mwaka 2025 kuwa na vituo zaidi ya 30 ",Amesema.

Aidha amesema kuwa gari hizo maalumu zitakuwa zinapaki katika maeneo mbalimbali ambapo watu watakuwa wanafika na kujaziwa gesi kwenye vyombo vyao vya moto.

Aidha akizungumzia Mradi wa ECOP amesema mradi huo umefikia asilimia zaidi 30 ambapo mpaka mwaka 2025 mradi utakuwa umekamilika

Sambamba na hayo Mhandisi Mramba ameitaka  kampuni tanzu ya TPDC(GASCO) kutumia maonesho hayo kujitangaza kwani watu wengi hawajui wanachokifanya kwani wanachofanya kina umuhimu na tija kubwa kwa maslahi ya umma.

"Kuna wawekezaji wengi ambao wanakuja hapa nchini kujenga vituo vya mafuta lakini sijui kama wanawajua nyinyi mpo mnapaswa kujitangaza na kuelezea kazi zenu mnazozifanya ili watu hawa wanapokuja wakutane na nyinyi",Amesema.

RAIS SAMIA AFANYA UFUNGUZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA WILAYA YA KALAMBO RUKWA.

RAIS SAMIA AFANYA UFUNGUZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA WILAYA YA KALAMBO RUKWA.

RAIS SAMIA AELEZA JITIHADA ZA KUFUNGUA MKOA KATAVI KWA MIUNDOMBINU YA BARABARA

RAIS SAMIA AELEZA JITIHADA ZA KUFUNGUA MKOA KATAVI KWA MIUNDOMBINU YA BARABARA

DKT. MPANGO AIPONGEZA WIZARA YA NISHATI KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA NISHATI

DKT. MPANGO AIPONGEZA WIZARA YA NISHATI KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA NISHATI

MWELI AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA KATIKA MIRADI YA KILIMO.

MWELI AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA KATIKA MIRADI YA KILIMO.

EWURA YAHAMASISHA MATUMIZI YA GESI ASILIA KWENYE VYOMBO VYA MOTO.

EWURA YAHAMASISHA MATUMIZI YA GESI ASILIA KWENYE VYOMBO VYA MOTO.