MPOTO AIPONGEZA SERIKALI MAONESHO YA 48 SABASABA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

MPOTO AIPONGEZA SERIKALI MAONESHO YA 48 SABASABA.

MSANII wa nyimbo za asili ya Mtanzania Mrisho Mpoto ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongezi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu hali iliyopelekea kuvutia uwekezaji.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
08 Jul 2024
MPOTO AIPONGEZA SERIKALI MAONESHO YA 48 SABASABA.

MSANII wa nyimbo za asili ya Mtanzania Mrisho Mpoto ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongezi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu hali iliyopelekea kuvutia uwekezaji.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Maonesho ya 48 ya biashara amesema ongezeko la makampuni mengi ya nje umechochewa na mazingira mazuri yaliyowekwa na Serikali.

Amesema maonesho ya mwaka huu yamekuwa na utofauti mkubwa na miaka mingine kwani miundombinu ndani ya maonesho imeimarika.

"Awali hapa tulikuwa ukija sabasaba unatoka na vumbi mpaka kichwani lakini sasa hivi unakuja huku unafurahia mpaka unatoka barabara zote zinarami mitaa inaonekana"Amesema Mpoto.

Sambamba na hayo Mpoto amewapongeza Wakala wa Nishati Vijijini REA kwa kuhakikisha vijiji vyote nchini vinakuwa na huduma ya umeme kwani utaenda kutatua changamoto ya umeme lakini pia utachochea matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Amesema uwepo wa umeme wa REA vijijini umekuwa chanzo cha ukuaji wa uchumi kwa wananchi waishio huko lakini pia unaenda kutekeleza kwa vitendo lengo la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan la matumizi ya nishati safi ya kupikia.

"REA inafanyakazi kubwa na imebeba ajenda ya Rais samia ya kuhakikisha ifikapo 2030 nchi inakuwa inatumia nishati safi ya kupikia kwani watu wakianza kutumia nishati hiyo itasaidia kutunza mazingira",Amesema.

FCC YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA KUTOKOMEZA BIDHAA BANDIA.

FCC YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA KUTOKOMEZA BIDHAA BANDIA.

TRA YAENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA SERIKALI KUHUSU WAFANYABIASHARA.

TRA YAENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA SERIKALI KUHUSU WAFANYABIASHARA.

NIC YAENDELEZA UBABE YASHIKA NAFASI YA KWANZA KWA MARA TATU MFULULIZO.

NIC YAENDELEZA UBABE YASHIKA NAFASI YA KWANZA KWA MARA TATU MFULULIZO.

WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI.

WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI.