TPDC KUTOA ELIMU KWA WANANCHI SABASABA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

TPDC KUTOA ELIMU KWA WANANCHI SABASABA

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)limeendelea kutoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda lao Katika Maonyesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), wakitaka kujua zaidi kuhusu matumizi ya gesi asilia.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
08 Jul 2024
TPDC KUTOA ELIMU KWA WANANCHI SABASABA

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)limeendelea kutoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda lao Katika Maonyesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba),  wakitaka kujua zaidi kuhusu matumizi ya gesi asilia.

Akizungumza na kwenye maonyesho hayo Afisa Uhusiano wa TPDC, Francis Lupokela,amesema kuwa wananchi wengi wameonesha nia kubwa ya kujua jinsi gesi asilia inavyoweza kutumika katika maisha yao ya kila siku ikiwamo na viwanda.

“Katika maonyesho haya, tumeona mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi wanaotaka kufahamu zaidi kuhusu matumizi ya gesi asilia. Wananchi wanataka kujua jinsi ya kutumia gesi asilia majumbani mwao na pia katika shughuli za kibiashara.

“Wengi wao wanatamani kuona upatikanaji wa gesi asilia ukiongezeka katika sehemu mbalimbali hatua mbayo wanaamini kuwa itaweza kuwaokolea gharama na kutunza mazingira jambo ambalo sisi TPDC tumelipokea,” amesema Lupokela.

Lupokela alieleza kuwa matumizi ya gesi asilia yana faida nyingi ikiwemo kupunguza gharama za nishati na kusaidia kuhifadhi mazingira. Alibainisha kuwa TPDC imejipanga kuhakikisha gesi asilia inafikishwa kwa wananchi wengi zaidi kwa gharama nafuu.

“TPDC imejipanga kuhakikisha tunafikisha gesi asilia kwa wananchi kwa gharama nafuu na kwa usalama. Tunaendelea na jitihada za kuongeza miundombinu ya kusambaza gesi ili iweze kuwafikia wananchi wengi zaidi,” aliongeza Lupokela.

Katika banda hilo, wananchi mbalimbambali walipata fursa ya kuona mifano ya matumizi ya gesi asilia katika kupikia, kuendesha magari, na kuendesha mitambo mbalimbali ya viwandani. Pia walipata elimu kuhusu usalama wa matumizi ya gesi asilia na jinsi inavyoweza kuboresha maisha yao ya kila siku.

“Haya maonyesho ni fursa muhimu kwa wananchi kupata elimu na kujua zaidi kuhusu gesi asilia. Tunawahimiza watembee katika banda letu ili wapate taarifa sahihi na kujionea wenyewe manufaa ya gesi asilia,” alisema Lupokela.

“Elimu niliyoipata hapa imenisaidia kuelewa jinsi gesi asilia inavyoweza kupunguza gharama za nishati na kuchangia katika kuhifadhi mazingira, hivyo elimu hii ni muhimu iwapo itawafikia watu wengi zaidi ili kuchochea utunzaji wa mazingira,” alisema mmoja wa wakazi hao.

Maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea yamekuwa ni jukwaa muhimu kwa TPDC kuwasilisha huduma na bidhaa zake kwa wananchi, huku ikiendelea na jitihada za kuongeza ufahamu na matumizi ya gesi asilia nchini.

NYONGO AZITAKA ASASI ZA KIRAIA KUFANYA MAJADILIANO YA PAMOJA ILI KUFANIKISHA DIRA YA MAENDELEO 2050.

NYONGO AZITAKA ASASI ZA KIRAIA KUFANYA MAJADILIANO YA PAMOJA ILI KUFANIKISHA DIRA YA MAENDELEO 2050.

DKT.BITEKO AIPONGEZA TPDC KWA UJENZI WA VITUO VYA CNG.

DKT.BITEKO AIPONGEZA TPDC KWA UJENZI WA VITUO VYA CNG.

DKT.BITEKO ATOA WIKI MOJA KWA TANESCO KUBORESHA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA.

DKT.BITEKO ATOA WIKI MOJA KWA TANESCO KUBORESHA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA.

Mitungi 19,530 kuuzwa kwa bei ya ruzuku kwa lengo la kuhamasisha na kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia

Mitungi 19,530 kuuzwa kwa bei ya ruzuku kwa lengo la kuhamasisha na kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia

NECTA:WALIOFELI KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE KURUDIA DARASA.

NECTA:WALIOFELI KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE KURUDIA DARASA.