

Makamu wa Rais, Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango ameipongeza Wizara ya Nishati kwa usimamizi madhubuti wa miradi mbalimbali ya Sekta ya Nishati hususan miradi ya umeme ambayo inapelekea nchi kuzidi kujiimarisha kiuchumi.
Dkt. Mpango ametoa pongezi hizo leo leo Julai 8, 2024 wakati alipokagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Kigoma yenye urefu wa Kilomita 395 pamoja na ujenzi wa kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme cha Nguruka na na Kidahwe vilivyoko mkoani Kigoma.
Akiwa kwenye kituo cha kupoza umeme cha Nguruka ambacho ujenzi wake umefikia asilimia 95, Dkt. Mpango ameiagiza Wizara ya Nishati kupitia TANESCO kuhakikisha ifikapo mwezi Septemba mwaka huu Kigoma iwe imeungwa kwenye Gridi ya Taifa ya umeme na hivyo kutatua changamoto ya upatikanaji wa umeme ambao umekuwa ukirudisha nyuma shughuli za uwekezaji kwenye mkoa huo.
‘’Nimpongeze Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko kwa kuisimamia vyema sekta hii, na pia niwapongeze sana TANESCO kwa kazi nzuri mnayofanya ila ni muhimu sasa mkahakikisha Mkoa wa Kigoma unaingia kwenye Gridi ya Taifa ili kuufungua mkoa huu kiuchumi." Amesema Dkt Mpango
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amemshukuru Makamu wa Rais, kupitia Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha za kutosha kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali hususan mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nguruka na kuahidi kuendelea kusimamia miradi ya nishati ili kuhakikisha umeme unapatikana kwa uhakika kwa wananchi.
‘’ Nikuhakikishie Mhe Makamu wa Rais sisi Wizara ya Nishati tunakuhakikishia kuwa hatutakuwa kikwazo kwa wananchi kupata umeme bali tunaahidi kuwapatia umeme wa uhakika watanzania wote’.’ Amesema Mhe Kapinga
Ameongeza kuwa Wizara itaendelea kutekeleza miradi ya umeme ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa mradi wa umeme wa Igamba Kidahwe hadi Malagarasi ambapo mpaka sasa mkandarasi ameshakabidhiwa eneo la mradi.
Mradi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Kigoma na kituo cha kupoza umeme cha Nguruka unatekelezwa na mkandarasi kampuni ya TBEA kutoka China na unagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 12 na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kidahwe kitakachopokea umeme kutoka Nyakanazi unagharimu shilingi bilioni 5 na unatekelezwa na wataalam wa ndani kutoka TANESCO.
.
Ujenzi huo ukikamilika utaunganisha Wilaya nne za Mkoa wa Kigoma ambazo ni Kigoma Mjini, Buhigwe, Uvinza na Kasulu na pia kuongeza hali ya upatikanaji wa umeme kwa mkoa wa Kigoma kupitia Gridi ya Taifa.
Waziri Mkuu Azindua Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini GovESB.
LUKUVI AWASILISHA BUNGENI TAARIFA YA HALI YA DAWA ZA KULEVYA
UDSM YASAINI MAKUBALIANO NA KAMPUNI ZA CHINA KUTOA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI WA CHUO HICHO.
WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA
MAONESHO YA UTALII NA UWEKEZAJI ZANZIBAR; FURSA KWA WANANCHI KUJUA VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO NGORONGORO
GRAND BUNGE BONANZA KUFANYIKA JUNI 21 2025 HUKU MGENI RASMI AKITARAJIWA KUWA RAIS SAMIA.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.