

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema itaendelea kuhamasisha matumizi ya gesi asilia katika vyombo vya moto ikiwemo magari ili kuendeleza matumizi ya nishati safi huku wito ukitolewa kwa wawekezaji kujikita katika uwekezaji wa vituo vya gesi hiyo –CNG.
SERIKALI kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema itaendelea kuhamasisha matumizi ya gesi asilia katika vyombo vya moto ikiwemo magari ili kuendeleza matumizi ya nishati safi huku wito ukitolewa kwa wawekezaji kujikita katika uwekezaji wa vituo vya gesi hiyo –CNG.
Pia,amesema wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhamasisha matumuzi ya nishati safi ya kupikia ili kuendana na Mkakati wa Kitaifa ambao umelenga kuhakikisha Watanzania wanahamia kwenye matumizi ya nishati hiyo ya kupikia.
Hayo yamebainishwa leo Julai 5,2024 na Meneja mawasiliano na uhusiano EWURA, Titus Kaguo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wao katika maonesho ya 48 ya biashara kimataifa yanayoendelea Jijini Dar es salaam.
"Tunawahamasisha wawekezaji wawekeze kwenye vituo vya ujazaji wa gesi asilia ambapo utaratibu umesharekebishwa na Shirika la viwango Tanzania(TBS )kwamba kituo cha mafuta kinaweza pia kuuza gesi asilia kwenye magari". Amesema Kaguo.
Sambamba na hayo Kaguo amesema –EWURA imekusudia kutumia maonesho hayo katika kutoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zinatolewa na mamlaka hiyo.
Amesema kupitia Maonesho hayo imekuwa fursa kukutana na wadau pamoja na wananchi kwa ujumla kutoa elimu kuhusu masuala ya petroli, umeme, gesi asilia pamoja na maji na usafi wa mazingira.
DKT. BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA CLIMATE INVESTMENT FUNDS
KAMATI ya Bunge ya miundombinu yaridhishwa na kasi ujenzi daraja la pangani
MIKOA 16 kunufaika na Nishati ya Jotoardhi
MASAA YA Upatikanaji wa Huduma ya Maji Yameongezeka Kutoka saa 16 hadi saa 22
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wadau wa kemikali
Hatua Kali Za Kisheria Kuchukuliwa Kwa Watakaoghushi Cheti Cha Kuhitimu Mafunzo ya JKT.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.