VETA YAPONGEZWA KWA KUJALI WENYE MAHITAJI MAALUM. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

VETA YAPONGEZWA KWA KUJALI WENYE MAHITAJI MAALUM.

Mamlaka ya Elimu na ufundi stadi VETA kimepongezwa kwa kujali na kutoa mafunzo ya ufundi stadi na ujasiliamali kwa watu wenye mahitaji maalumu kwani elimu hiyo imewasaidia kujikwamua na kuwafanya wasiwe tegemezi.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
05 Jul 2024
VETA YAPONGEZWA KWA KUJALI WENYE MAHITAJI MAALUM.

Mamlaka ya Elimu na ufundi stadi VETA kimepongezwa kwa kujali na kutoa mafunzo ya ufundi stadi na ujasiliamali kwa watu wenye mahitaji maalumu kwani elimu hiyo imewasaidia kujikwamua na kuwafanya wasiwe tegemezi.

Pongezi hizo zimetolewa leo julai 5,2024 na mwenyekiti wa baraza la NACTIVET Benadetha Ndunguru  kwenye maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es salaam .

Amesema amevutiwa kwa kuwaona watu wenye ulemavu wakiwa wanajishughulisha katika kazi mbalimbali ikiwemo kushona nguo na kuchonga.

"VETA mnafanya vizuri sana kwa kuwajali na kuwaendeleza watu wenye mahitaji maalumu kwani sasa hivi wanaweza kujitegemea nimeona vipofu wanashona nguo,wanachonga na kuendesha mashine mbalimbali za utengenezaji wa vifaa hii ni kitu muhimu sana na tunapaswa kuendelea kuwaunga mkono",Amesema.

Aidha ameongeza kuwa watu wenye uhitaji maalumu wakipatiwa ujuzi wa kutosha wanaweza kujiajili na kuendesha maisha yao.

Sambamba na Nduguru ametoa rai kwa wazazi kutowaficha na kukuaa nao nyumbani watu wenye ulemavu badala yake wawaendeleze kwa kuwapa elimu ikiwemo ya ufundi stadi ili waweze kujitengenezea maisha yao ya baadae.

DCEA YAMSHIKILIA MTENGENEZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.

DCEA YAMSHIKILIA MTENGENEZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.

JUKWAA LA KILIMO LAWAHIMIZA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KILIMO.

JUKWAA LA KILIMO LAWAHIMIZA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KILIMO.

WANANCHI WAJIANDAA KUSHUHUDIA UZINDUZI WA VIHENGE

WANANCHI WAJIANDAA KUSHUHUDIA UZINDUZI WA VIHENGE

REA:VIJIJI 151 KUFUNGIWA UMEME  KABLA YA SEPTEMBA.

REA:VIJIJI 151 KUFUNGIWA UMEME KABLA YA SEPTEMBA.

GEP YAZIPONGEZA TAASISI ZINAZOWEZESHA UPATIKANAJI WA HAKI.

GEP YAZIPONGEZA TAASISI ZINAZOWEZESHA UPATIKANAJI WA HAKI.