MAONESHO YA 48 YA BIASHARA KUFUNGULIWA KWA HISTORIA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

MAONESHO YA 48 YA BIASHARA KUFUNGULIWA KWA HISTORIA.

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa nchi ya Msumbiji, Filipe Nyusi wanatarajiwa kuzindua maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara julai 3,2024.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
02 Jul 2024
MAONESHO YA 48 YA BIASHARA KUFUNGULIWA KWA HISTORIA.

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa nchi ya Msumbiji, Filipe Nyusi wanatarajiwa kuzindua maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara julai 3,2024.

Akizungumza mara baada ya kutembelea maonesho hayo WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji amesema maonesho hayo yamekuwa ya Kimataifa kwa sababu waonyeshaji kutoka nje ya nchi wameongezeka tofauti na ilivyokuwa awali.

Amesema maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) ya mwaka huu  ni ya mfano wa kuigwa kwa sababu yamekidhi viwango vya kimataifa.

Waziri huyo amesema maonyesho hayo pia yatatoa fursa mbalimbali kwa Watanzania kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara wa ndani na nje.

Aidha ameongeza kuwa nchini 26 zimeshiriki maonyesho hayo ambazo zitaonyesha bidhaa zao mbalimbali .

Dk.Ashatu amesema tayari walishawaahidi  Watanzania kuwa nchini hii ni ya viwanda hivyo kwenye maonyesho hayo kuna viwanda vingi vimeshiriki lengo ni kubadilishana uzoefu.

Kwa upande wake, Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalailla amewakaribisha wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuhudhuria kwa wingi katikà ufunguzi wa maonyesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF).

Chalamila amesema katika ufunguzi huo kutakuwa na mabasi yaendayo kasi (UDART)ambayo yatafanya safari zake katika maneno ya Mbande,Chamazi na maeneo mengine ya mbagala lengo ni kutaka kila mwananchi aweze kufika katikà maonyesho hayo

"Maonesho haya yamebeba kauli mbiu mahususi ya kuwakaribisha wawekezaji wafike kwa wingi kuwekeza nchini ambayo inasema "Tanzania ni eneo sahihi salama kwa uwekezaji"amesema Chalamira

Akizungumzia suala la usafi katikà kipindi hicho Cha maonyesho hayo amesema wamejipanga kuhakikisha Wilaya yote ya Temeke inakuwa ni safi huku ikizingatia mabadiliko ya tabia ya nchini.

"Tunahakikisha suala la ulinzi na usalama linaimarishwa zàidi hivyo majambazi na wadokozi hawatakuwa na nafasi katikà maonesho haya pia camera tulizozifunga zitatusaidia kuwaona wahalifu wote,"amesema Chalamila.

FCC YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA KUTOKOMEZA BIDHAA BANDIA.

FCC YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA KUTOKOMEZA BIDHAA BANDIA.

TRA YAENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA SERIKALI KUHUSU WAFANYABIASHARA.

TRA YAENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA SERIKALI KUHUSU WAFANYABIASHARA.

NIC YAENDELEZA UBABE YASHIKA NAFASI YA KWANZA KWA MARA TATU MFULULIZO.

NIC YAENDELEZA UBABE YASHIKA NAFASI YA KWANZA KWA MARA TATU MFULULIZO.

WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI.

WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI.